.AFISA UGAVI ,
a. Sifa
- Awe na shahada au stashahada ya juu katika fani ya manunuzi na ugavi (materials management) kutoka katika chuo kinachotambuliwa na serikali
- Awe na cheti cha CPSP na awe amesajiliwa na PSPTB na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili
- Awe na umri wa kati ya miaka 25 na 45
- Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na mifumo ya fedha katika kompyuta (Accounting packages)
- Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili
b. Majukumu
- Atatakiwa kutambua mahitaji yabidhaa na huduma mbalimbali za kampuni na kufanya manunuzi kwa wakati muafaka na kwa gharama nafuu kwa kuzingatia sheria ya manunuzi na kanuni zake
- Kuwashauri viongozi wa kampuni kuhusu kanuni na taratibu sahihi za kufuata wakati wa kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma kwa ajili ya kampuni
- Kwa kusaidiana na viongozi wa kampuni kuweka kumbukumbu ya vifaa vilivyo chakaa, ambavyo havijachakaa na thamani yake
- Kuandaa makabrasha ya tenda, na kupokea na kuwasilisha tenda
- Kuhakikisha nyaraka zote za ununuzi na uuzaji zinapatikana na kujazwa vizuri kwa kuzingatia sheria na kanuni za ununuzi
- Kuhakikisha kwamba nyaraka zote za ununuzi na uuzaji zinatunzwa vizuri kwa ajili ya kumbukumbu pale zinapohitajika
- Atafanya kazi nyingine zozote kwa maelekezo ya manejimenti
Mwisho wa kupokea maombi ya kazi hizi ni Desemba 31,2016.
Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa:
Mkurugenzi Mkuu,
Boimanda Modern Construction Company Ltd,
S.L.P 1491,
Iringa.
EmoticonEmoticon