3. MHASIBU MSAIDIZI (Nafasi mbili)
a Sifa
- Awe tayari kufanya kazi ama katlka mkoa wa Iringa, Njombe au katika kituo chochoteatakachopangiwa na mwajiri
- Awe na stashahada (diploma) katika rnasomo ya uhasibu
- Awe na ufahamu wa kutosha kuhusu utaratibu, kanuni na sheria za makampuni
- Awe mbunifu, mwaminifu, anayejituma na anayeweza kujisimamia mwenyewe
- Awe na umri wa kati ya miaka 25 na 45 na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili
- Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na mifumo ya fedha katika kompyuta (Accountingpackages)
b. Majukumu
- Awe na uwezo wa kupokea na kulipa fedha
- Ajue namna yakutunza daftari la fedha
- Ajue kufanya usuluhishi wa hesabu za benki
- Ajue kukagua hati za malipo
- Ajue kupitisha malipo kulingana na kanuni za fedha
- Ajue namna ya kusimamia kazi za wasaidizi wa hesabu
- Atakuwa msaidizi wa mhasibu mkuu
Mwisho wa kupokea maombi ya kazi hizi ni Desemba 31,2016.
Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa:
Mkurugenzi Mkuu,
Boimanda Modern Construction Company Ltd,
S.L.P 1491,
Iringa.
EmoticonEmoticon